Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 5, 2019

Waziri Lugola Asema Tanzania Ipo Salama Na Imara

Na Mwandishi Wetu.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Tanzania ni kisiwa cha amani na pia ipo imara katika Bara la Afrika licha ya uwepo wa baadhi ya watu wachache wanaoichafua taswira yake kwa maslahi yao binafsi.

Lugola ameyasema hayo jijini Dodoma leo, alipokua anazungumza na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg, ofisini kwake alimueleza kuwa, Rais Dk John Magufuli anaendelea kuiongoza nchi vizuri, na mpaka sasa Tanzania ipo imara na itaendelea kuwa imara, na wageni mbalimbali wanakaribishwa kuja nchini kuwekeza, kufanya utalii pamoja na masuala mbalimbali ambayo yatawezesha nchi kupata maendeleo zaidi.

“Mheshimiwa Balozi nchi yetu ipo salama na tunaendelea kuijenga kwa juhudi zote, Sweden na Tanzania ni marafiki kwa miaka mingi, yangu kipindi cha uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, hivyo tutaendelea kushirikiana nanyi ipasavyo, nakukaribisha sana Dodoma na hapa ndio makao makuu ya nchi,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, anaikaribisha Serikali ya Sweden pamoja na wananchi wake wafike nchini kuwekeza katika maeneo mbalimbali yakiwemo utalii, pamoja na masuala ya biashara.

Waziri na Balozi huyo, pia walijadiliana masuala ya ushirikiano katika kuendelea kuimarisha usalama nchini, huku Lugola akimwambia Balozi huyo mikakati ya nchi katika kuimarisha ulinzi ambapo Serikali inatarajia kufunga kamera usalama (CCTV) katika Jiji la Dar es Salaam, Mwanza na Arusha kwa lengo la kuimarisha ulinzi zaidi.

Waziri Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini.

“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.

Hata hivyo, Balozi Sjoberg alifurahi kuonana na Waziri huyo pamoja na kufika Makao Makuu ya Serikali jijini Dodoma ikiwa ni mara yake ya pili tangu alipofika nchini kwa ajili ya kuiwakilisha nchi yake, pia alimuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Sweden na Tanzania.
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )