Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 9, 2019

Waziri Mkuchika Atoa ONYO Kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya Wanaowasweka Watu Rumande

juu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika, amewaumbua baadhi ya wakuu wa Wilaya nchini wanaowaweka ndani watu kwa saa 48 wakati hakuna sheria inayowapa mamlaka hayo.

Mkuchika amewataka wakuu hao wa Wilaya kuacha kutumia mabavu kwenye utendaji wao wa kila siku kwa kuwa wakiendelea na tabia hiyo watakuwa wanahatarisha kazi yake ya uwaziri.

Aliyasema hayo juzi bungeni wakati akichangia na kueleza kuwa wakuu wa wilaya na mikoa wanapaswa kutumia busara katika kuwaweka ndani raia.

“Msiniponze. Mimi nataka Rais Magufuli asinibadili hapa, mimi nataka Rais Magufuli aseme mzee endelea, tuache masuala ya umwamba, nawaomba huko mliko msiniharibie kazi yangu. Mimi ndiye mwenye cheo cha utawala bora, mimi ndiye waziri mwenye dhamana ya utawala bora, ukiendesha mambo kinyume cha utawala bora unaniharibia kazi,” alisema Mkuchika.

Alisema madaraka ya wakuu wa wilaya kuwaweka ndani watu saa 24, lugha iliyotumika ni kwa usalama wake, maana yake mtu ameua mtu na jamaa zake wamekasirika wanataka kumpiga yule aliyeua na hapo ndipo dhana ya kumweka huyo mtuhumiwa ndani saa 24 inatumika kwa usalama wake.

Alisema mkuu wa wilaya akishamweka mtu huyo ndani ya saa 24 na muda huo ukamalizika, ikifika asubuhi ni lazima apelekwe mahakamani.

“Nataka niseme mahali popote mkuu wa wilaya kumweka ndani mtu saa 48 ni makosa kwa sababu sheria inampa saa 24 na mkuu wa mkoa amepewa saa 48,” alisema Mkuchika.

Aliongeza kuwa mkuu wa mkoa amepewa mamlaka ya saa 48 na akipenda anaweza kumweka mtuhumiwa ndani saa 24 na si lazima amweke mtu ndani.

“Kama ni kosa la jinai OCD (Mkuu wa Polisi wa Wilaya) yuko. Kama ni suala la uhamiaji mtu wa uhamiaji yupo, kama amekwepa kodi mtu wa TRA (Mamlaka ya mapato Tanzania) yupo, si lazima utamke wewe,” alisema Mkuchika.

chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )