Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 24, 2019

Waziri Mkuu Asema Haridhishwi na Hali ya Kiusalama Katika Mpaka wa Holili baina ya Tanzania na Kenya

juu
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameeleza kutoridhishwa kwake na hali ya kiusalama katika mpaka wa Holili baina ya Tanzania na Kenya na kutaka vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza ushirikiano kudhibiti uingiaji holela wa watu na bidhaa.

Amesema hayo wakati akikagua shughuli za kituo cha Forodha Holili kujua changamoto zao lakini pia kutoa maelekezo ya serikali nini kifanyike kuhakikisha taifa linaendelea kuwa salama.

Waziri mkuu alisema anazo taarifa kwamba mpaka huo huingizwa baadhi ya bidhaa na watu ambao huingia kwa njia tofauti, jambo ambalo alisema linakuwa tishio la kiusalama.

“Lazima majeshi yetu kwa nchi za Tanzania na Kenya kwa kushirikiana na idara ya uhamiaji wakajiridhisha kuhusu utendaji wao na kuanzisha mfumo wa pamoja wa kiusalama ili kuhakikisha hakuna mtu anayeingia Kenya ama Tanzania na kufanya uhalifu wa aina yoyote,” alisema.

Alitaka kitengo kinachohusika na ukaguzi na mizigo na vifurushi katika mpaka wa Holili kuwa waadilifu na wenye kutumia teknolojia kubaini bidhaa na silaha ambazo zingeweza kupitishwa kwa ujanja ujanja katika mpaka huo na kwenda kuleta athari Tanzania au Kenya.

“Lazima ninyi maofisa uhamiaji na majeshi yetu mliopo hapa mpakani mtumie mbinu zote kubaini uhalifu wowote ambao unaweza kufanyika, mpaka huu una njia za Panya zaidi ta 260...wengine wanaweza kupita kwa vibali halali lakini ndani ya mizigo yao kuna silaha na hata mabomu,” alisema.

Aidha waziri mkuu alitaka majeshi yaliyopo mpakani hapo kushirikiana vyema kudhibiti uhalifu lakini pia aliwataka wananchi kufuata sheria pale wanapotaka kwenda upande mwingine wa nchi kwani kinyume na hapo watajiingiza matatani na hakutakuwa na msamaha.

“Yapo ambayo yalitokea kwa wenzetu Kenya na wote mliyasikia...sasa tusipokua makini tunaweza kuvuruga mahusiano baina ya nchi zetu, kwani tunaweza kutuhumiana iwapo mhalifu atapita mpakani kuelekea nchi nyingine na kufanya uhalifu wowote,” alisema.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )