Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 7, 2019

Waziri wa Madini Doto Biteko Akutana Na Watumishi Tume Ya Madini

juu
Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 06 Februari, 2019 amekutana na watendaji na watumishi wa Tume ya Madini katika makao makuu ya Tume yaliyopo jijini Dodoma, lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Tume.

Kikao hicho  kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mkurugenzi wa  Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi na  Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula.

Wengine ni pamoja na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, Wakurugenzi, Mameneja pamoja na watumishi wa  Tume ya Madini.

Katika kikao hicho Waziri Biteko ametoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vituo vya ukaguzi wa madini ya ujenzi kufufuliwa, kikao cha kamati tendaji kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kupitia na kuidhinisha maombi mbalimbali ya leseni za madini na watumishi kufanya kazi kwa uadilifu.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )