Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 22, 2019

Wema Sepetu akana kuchapisha video ya ngono Mtandaoni

juu
Msanii wa Filamu Nchini, Wema Sepetu (30) amekana mahakamani tuhuma za kuchapisha video ya ngono katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.

Hata hivyo, Wema amekiri majina na anuani yake wakati akisomewa maelezo ya awali jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Maelezo hayo yalisomwa mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Wakili wa Serikali, Glory Mwenda, alidai kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili kusikiliza maelezo ya awali dhidi ya mshtakiwa.

Wakili wa utetezi, Ruben Simwanza, alidai utetezi wako tayari kusikiliza maelezo hayo. Mwenda alidai kuwa Wema anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono katika mtandao wa jamii wa Instagram.

Alidai kuwa kutenda Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, alitenda kosa hilo la kusambaza video za ngono kupitia ukurasa wake ya Instagram, picha zisizokuwa na maudhui.

Wakili huyo, alidai Wema ambaye ni mkazi wa Mbezi Salasala, anamiliki ukurasa katika mtandao wa jamii wa Istagramu wenye jina la Wemasepetu.

Alidai siku hiyo ya tukio, mshtakiwa alirekodi video ya ngono ambayo haina maudhui kupitia simu yake ya kiganjani, akitumia laini ya Vodacum yenye namba 0755 555 ***.

Baada ya kurekodi video hiyo, Oktoba 25, 2018, mshtakiwa huyo aliisambaza katika akaunti yake ya Istagram, wakati akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Glory alidai kuwa video hiyo aliyorekodi Wema, ilikuwa inaonyesha kuwa Wema alikuwa ananyonyana ndimi (denda) na mwanaume, huku akijua kuwa kitendo hicho ni kinyume na maadili ya Tanzania.

Hata hivyo, Oktoba 25, 2018 maofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA), waliiona video hiyo na kuripoti tukio hilo katika kituo cha Polisi Kijitonyama.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa, baada ya maofisa wa TCRA kuripoti tukio hilo, Wema alikamatwa Oktoba 29, 2018 na kupelekwa katika kituo cha Kikuu cha Polisi (Central), ambapo alihojiwa na polisi.

Baada ya kuhojiwa polisi, Wema alikana kuhusina na tukio hilo na Novemba Mosi, 2018, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kufunguliwa shtaka moja ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii.

Baada ya kusomewa maelezo hayo, alikubali majina yake mawili, anuani yake na sehemu anayoishi.

Pia alikubali kuwa anamiliki akaunti ya Istagram yenye jina la Wemasepetu.

Alikiri kukamatwa Oktoba 29, 2018 na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuhojiwa, alifikishwa Mahakama ya Kisutu, Novemba Mosi, 2018, kujibu shtaka linalomkabili.

Hata hivyo, upande wa mashtaka ulidai kuwa unatarajia kuwa na mashahidi watano katika kesi hiyo.

Hakimu Kasonde alisema kesi hiyo itaanza kusikiliza mashahidi wa Jamhuri Machi 18, mwaka huu.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )