Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 15, 2019

Zaidi Ya Bil. 16.324.9 Zimelipwa Kwa Wakulima Wa Korosho Mkoani Pwani

juu
Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji 
JUMLA ya kilo 5,623,277 za korosho zenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 16.324.9 tayari zimelipwa kwa wakulima mkoani Pwani.

Aidha wakulima wa korosho 24,543 ,wenye kilo 14,370, 844 kati ya kilo 21,130,598 zilizopo kwenye maghala makuu wameshakikiwa, sawa na asilimia 68 .

Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Ndikilo alitoa taarifa hiyo wakati alipokuwa akizungumza kwenye ziara yake wilaya ya Mkuranga na Rufiji.

Alisema, zoezi la uhakiki lilikuwa mwisho february 15 lakini mkoa huo unaomba kuongezewa muda hadi february 28 mwaka huu, kwakuwa umechelewa kuanza zoezi hilo na bei ya daraja la pili ilichelewa kutoka ambayo itakuwa sh. 2,640 kwa kilo .

Ndikilo alieleza, hadi tarehe 12 februari, mwaka huu jumla ya kilo 23,066,238 za korosho zimekusanywa, ambapo kilo 21,130,598, sawa na asilimia 91.6 zipo kwenye maghala makuu.

"Ghala kuu la Mwanambaya zipo kilo 6,549,204, Kibiti kilo 2,650,529, TANITA kilo 1,705,621, Kurasini PISAH kilo 3,727,669, Kurasini SCALABLE kilo 6,325,237 ,Kiegeani- Mafia kilo 213,593 na kilo 6,488,690 zipo kwenye maghala madogo ya AMCOS"alibainisha Ndikilo.

Nae katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji, Shangwe Twamala alisema mkoa wa Pwani ulichelewa kuanza ukusanyaji wa korosho tarehe 30 Oktoba, 2018 tofauti na mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma, ambayo ilianza mapema.

"Baadhi ya korosho kuendelea kuwepo kwenye maghala ya AMCOS, Ili kutatua changamoto hii, tunashauri malipo kwa wasafirishaji yafanyike kwa wakati ili waweze kufanya kazi hii"

"Kama itawezeakana tutumie magari ya jeshi kuhamisha korosho kutoka kwenye AMCOS kwenda maghala ya Kurasini"alieleza Twamala. Kwa upande wao mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga alisema, tani zaidi ya 4,000 za korosho kati ya 6,000 walizokusanya zipo chini ya sakafu ambapo wamezitandikia maturubai lakini wanahofia unyevunyevu zisije kuharibika.

Mkuu wa wilaya ya Rufiji Juma Njwayo alisema, wakulima wilayani hapo wamelipwa korosho sh. bilioni 3.7 ,kwa wakulima 2,665.#
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )