Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 19, 2019

Zamaradi aguswa na Suala la matibabu ya Ruge....Awahamasisha Watanzania Wamchangie

juu
Mtayarishaji wa vipindi, na mzazi mwenza wa Ruge Mutahaba,  Zamaradi Mketema leo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameunga mkono kampeni ya kumchangia Mkurugenzi wa Vipindi vya Clouds Media, Ruge Mutahaba ambaye yupo Afrika Kusini kwa matibabu.

Jana kwenye mahojiano na Clouds TV kwenye kipindi cha 360 mdogo wa Ruge, Mbaki Mutahaba alieleza kuwa Ruge anasumbuliwa na tatizo la figo ambalo limepelekea matibabu yake kuwa ya gharama zaidi kuliko kawaida ambapo amesema kwa siku anaweza kutumia milioni 5 hadi 6 kwa ajili ya matibabu pekee.

Mapema leo Zamaradi Mketema ameunga mkono kampeni hiyo kwa kuwataka watu mbalimbali kutuma jumbe za faraja na wenye chochote kutuma kwenye namba ya mdogo wa Ruge, kwani gharama za matibabu ya Ruge zimekuwa kubwa sana kuliko kawaida.

”Mbaki Mutahaba ambae ni mdogo wa Ruge Mutahaba ameeleza kwamba ni wazi kwamba gharama za matibabu ya Ruge ni kubwa mno. Amesema Rais Dkt Magufuli na wengine walichangia lakini gharama  hizo ni kubwa kuliko kawaida. ”Gharama za matibabu kwa kule ni kubwa kwa siku inaweza kufika milioni 5 mpaka 6, kuna namba ambayo imeandikishwa kwa jina la mdogo wake, Kemilembe Mutahaba  0752 222 210 hiyo ndiyo namba ambayo watu wanaweza kutuma sms za pole, faraja na hata wengine ambao wangetamani kutuma chochote.” Mbaki Mutahaba.-Ameandika Zamarad
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )