Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, March 4, 2019

Alichokisema Balozi Agustine Mahiga Baada ya Kuapishwa Leo Kuwa Waziri Katiba na Sheria

juu
Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Dk Agustine Mahiga amesema wizara aliyokuwa akiihudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilikuwa inafanana na uzoefu wa kazi aliyokuwa akiifanya lakini sasa amepewa kazi ambayo ataifahamu zaidi nchi yake.

Mahiga ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Machi 4, 2019 mara baada ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema alikuwa na nafasi ya kubaki kuitumikia jumuiya ya kimataifa lakini yeye na familia yake waliona ni bora kurudi nyumbani.

"Nimefanya kazi katika jumuiya ya kimataifa kwa miaka 30, nimerudi nchini mwaka 2015 nikapewa ubunge na uwaziri, namshukuru sana Rais (John Magufuli)," amesema.

Amesema nchi yoyote lazima ijenge nafasi ya kulinda nafasi yake katika jumuiya za kimataifa na Tanzania ina marafiki wengi, hakuna maadui na hii ilitokana na sera yake nzuri ya kutofungamana na upande wowote.

"Hivi karibuni tulikuwa na malumbano na baadhi ya watu na mshirika lakini baada ya kuwaeleza kuhusu sera zetu walielewa," amesema.

Amesema katika utawala wake amekataa mialiko 30 na ameshiriki kutengeneza katiba ya nchi tano na anaona sasa ni wasaa mzuri kwake kuijua katiba ya nchi yake.

"Nashukuru kwa afya nilikuwa na safari nyingi wakati mwingine nilikuwa nabadilisha nguo airport (uwanja wa ndege) na kwa mwezi naonana na familia yangu mara mbili tu,” amesema Dk Mahiga.

Amesema ofisi yake mpya inampa nafasi ya kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali na wananchi hata utoro bungeni utapungua.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )