Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, March 14, 2019

Boeing 737 Max: Kampuni ya Marekani inayotengeneza ndege iliyoanguka Ethiopia yasitisha matumizi ya ndege zote aina hiyo

juu
Kampuni ya Boeing Marekani inayotengeneza ndege iliyoanguka Ethiopia imesitisha matumizi ya ndege zote aina hiyo baada ya wachunguzi kubaini ushahidi mpya katika eneo ambako ndege ya Ethiopia Airlines ilianguka.

Kampuni hiyo ya Marekani imesema itasitisha usafiri wa ndege zote 371 zinazohudumu.

Shirika linalosimamia usafiri wa anga Marekani FAA, limesema ushahidi mpya pamoja na data mpya za satelaiti zimechangia uamuzi huo wa kupiga marufuku kwa muda usafiri wa ndege hizo.

FAA awali lilisisitiza ndege ya Boeing 737 Max 8 ni salama wakati mataifa mengine yakipiga marufuku usafiri wa ndege hizo.

Ajali hiyo siku ya Jumapili mjini Addis Ababa ulisababisha vifo vya watu 157.

Ni ajali ya pili kuwahi kushuhudiwa ya ndege hiyo chapa Max 8 katika miezi mitano baada ya ajali nyingine nchini Indonesia mwaka jana Oktoba iliosababisha vifo vya watu 189.

FAA lina kundi la maafisa wanaochunguza mkasa huo katika eneo ambapo ajali ya shirika la ndege la Ethiopia ilipotokea likishirikiana na bodi ya kitaifa ya usalama wa safari.

Dan Elwell, kaimu msimamizi katika shirika hilo FAA, amesema Jumatano: " Imebainika wazi kwa pande zote kwamba safari ya ndege ya Ethiopia ilikaribiana na namna ilivyoshuhudiwa kwa ndege iliyoanguka awali ya Lion Air ."

Ameongeza kwamba "ushahidi tuliopata katika eneo, umefanya kuwa na uwezekano mkubwa kwamba hata njia ya ndege ilikaribiana na ile ya Lion Air".

Rais Donald Trump awali alitangaza kwamba shirika la FAA litatoa tangazo la dharura kufuatia "taarifa mpya na ushahidi tuliopokea kutoka eneo la mkasa na kutoka maeneo mengine kupitia malalamiko mengine tofauti".

Marekani ni nchi ya hivi karibuni kusitisha usafiri wa ndege hiyo ya Boeing 737 Max yakiwemo mataifa mengine kama Uingereza, Umoja wa Ulaya, China India na Australia ambayo yote yameamua kusitisha usafiri wa ndege hizo.


-BBC
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )