Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, March 21, 2019

Simba Kuivaa TP Mazembe Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika

Simba  imepangwa kuumana na TP Mazembe ya DRC  katika mchezo wa  hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wataanzia nyumbani, Uwanja wa Taifa, Dar es Dar  es Salaam Aprili 4.

Droo ya hatua hiyo ya robo fainali iliyohusisha timu nane, ilichezeshwa jana usiku Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), jijini Cairo, Misri.

Timu nyingine zilizoingia katika droo hiyo ni  Horoya ya Guinea itakayoumana na Wydad  Casablanca ya Morocco, Constantine ya Algeria itakayopepetana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Esperance ya Tunisia na  Mamelody Sundown ya Afrika Kusini itakayooneshana umwamba na Al Ahly.

Mshindi kati ya Mazembe na Simba atafuzu nusu fainali na kukutana na mbabe kati ya Constantine na Esperance, wakati mshindi kati ya Mamelod Sundowns na Al Ahly atapambana na mshindi kati ya Wydad Casablanca na Horoya.

Mara ya mwisho Simba na Mazembe zilikutana raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2011. Mchezo wa kwanza Wekundu hao walilala mabao 3-1 jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kabla ya kufungwa tena mabao 3-2 nyumbani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )