Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, March 18, 2019

Uongozi Wa Vyama Vya Wachimbaji Wadogo Usiingiliwe-

juu
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewaagiza watendaji wa Wizara ya Madini, Mikoa na Kamati za Ulinzi na Usalama wasimamie vyama vya wachimbaji wadogo na wahakikishe uongozi wake hauingiliwi na wachimbaji wa kati kwa lengo la kuepusha migogoro.

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Madini ishirikiane na vyama na mashirikisho ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuandaa Mpango Kazi mahsusi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya soko madini la Geita ili lisigeuke kuwa kikwazo kipya kwa wachimbaji na wafanyabishara wa madini.

Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo jana jioni (Jumapili, Machi 17, 2019) wakati akifungua soko la madini la Mkoa wa Geita. Ufunguzi wa soko hilo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilotoa tarehe 22.01.2019 la kuitaka mikoa yote ianzishe masoko ya madini.

Alisema mara kadhaa wachimbaji wadogo  wamekuwa wanalalamikia wachimbaji wa kati kuwaingilia na kutaka kuongoza vyama vyao pale wanapovianzisha jambo ambalo limekuwa likisababisha migogoro ya mara kwa mara baina yao.

“Hasa pale wachimbaji wadogo wanapokuwa wameunda uongozi, wachimbaji wa kati huanzisha mgogoro ili washike wao. Iko migogogro inapangwa kufanyika: Nyakafuru, Ikuzi, Bingwa na Gasuma. Wachimbaji wadogo waachwe waunde uongozi wao”.

Akizungumzia kuhusu kuanzishwa kwa soko hilo, Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali kuanzisha masoko ya madini ni zuri na lina maslahi mapana ya nchi. “Hivyo ni vyema tukahakikisha kwamba kwa pamoja, tunayalinda masoko haya, tunayatetea na tunayawezesha kwa kadri tunavyoweza”.

Alisema kwa upande wa Serikali, itahakikisha masoko haya yanaendeshwa kwa njia shirikishi, uwazi na uadilifu ili wote kwa pamoja wanufaike nayo, hivyo alizitaka Idara na Taasisi zote za Serikali zinazohusika na uwekaji wa miundombinu wezeshi kwenye soko hilo, zishirikiane na Wizara ya Madini ili soko hilo liweze kustawi.

Awali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alisema mikoa yote nchini imeshaanza taratibu za uanzishaji masoko ya madini ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo na majengo yatakayotumika kwa masoko hayo na baadhi ya mikoa hiyo ipo katika hatua za mwisho kukamilisha.

Alisema mkoa wa Geita hadi kufikia Februali mwaka huu una leseni kubwa za uchimbaji wa madini mbili, leseni za uchimbaji wa kati 48 na leseni za uchimbaji mdogo 1,119, leseni za uchenjuaji wa madini ya dhahabu 47, leseni kubwa za biashara ya madini ya dhahabu saba huku leseni ndogo zikiwa 113.

“Hii inaonesha kwa kiasi gani soko hili lilikuwa linahitajika sana hapa. Aidha kutoka katika mkoa huu wa Geita, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini, inaendelea kupitia maombi 258 ya leseni za uchenjuaji, maombi 12 ya leseni kubwa za biashara ya madini ya dhahabu na za maombi madogo zikiwa 86.”

Akizungumzia upande wa makusanyo, Profesa Msanjila alisema maduhuli yatokanayo na uzalishaji wa madini yameongeza katika mkoa huo kutoka sh. bilioni 24.56 mwaka 2010/2011 hadi kufikia sh. bilioni 114.78 mwaka 2017/2018. Ongezeko hilo ni muitikio chanya wa mabadiliko ya kisera na kisheria yaliyofanywa.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )