Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, March 11, 2019

Vyama Vya Ushirika Vyatakiwa Kuwa Na Mipango Yenye Tija

juu
Na Amiri kilagalila
Shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania (TFC) limesema kuwepo kwa mipango yenye kuleta tija katika vyama vya msingi vya ushirika nchini, ndiyo sababu mojawapo itakayowajengea imani na matumaini wananchi ya kujiunga na ushirika hivi sasa.

Meneja wa elimu na mafunzo kutoka shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania, FROLIAN HAULE ametoa kauli hiyo  baada ya kutembelea Kiwanda cha kusindika unga wa Sembe cha chama kikuu cha ushirika mkoa wa Njombe (NJORECU) akiwa ameongozana na ujumbe wa shirikisho hilo na kusema kuwa mfano mzuri uliofanywa na Njorecu unapaswa kuigwa na vyama vingine.

Chama Kikuu cha ushirika Mkoani Njombe (NJORECU) kimeanzisha kiwanda cha kusindika unga wa sembe unaotokana na malighafi ya mahindi ambapo shirikisho la vyama vya ushirika nchini limetoa wito kwa vyama vingine kuzingatia ushauri na elimu wanayokuwa wakiitoa katika mafunzo na kuvitaka vyama vikuu kuwa na viwanda vitakavyosaidia kujiendesha na kupata faida kubwa.

“Tayari kuna baadhi ya vyama vimekwisha chukua hatua za kuanza kufanya maswala ya uwekezaji hii inatia faraja na kwa msingi huo tunakuwa na darasa kwa vyama vingine kuja kujifunza kuwa uwekezaji kwa vyama vya ushirika unawezekana”alisema FROLIAN HAULE meneja wa mafunzo na elimu

Mwenyekiti wa chama kikuu mkoa wa Njombe NJORECU CLEMENT MALEKELA anasema kiwanda cha kuchakata unga wa sembe kilichogharimu kiasi cha shilingi Milioni 75 kimeleta faraja kwa wanachama hivi sasa ambao wameonyesha nia ya kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na viongozi, ikiwemo   kuanza kupata soko la kuuza unga wa sembe katika nchi jirani.

“Soko la nje tayali tumelifanyia utafiti kwa mfano tumetembelea Lwanda tukitafuta soko la Sembe ilionekana kikwazo kikubwa ni swala la ubora lakini kwa ujumla tunakwenda vizuri”alisema Malekela

Pamoja na vyama vya msingi vya ushirika kuanzisha viwanda vya kusaidia kujiendesha JOAN KIRWAY ambaye ni msimamizi wa kitengo cha bima za mikopo kwenye shirikisho hilo anasisitiza umuhimu kwa vyama vya ushirika kuwa na bima za mikopo ili kusaidia kuepukana na majanga ya aina mbalimbali.

“Lakini changamoto kubwa vyama vya ushirika mpaka sasa hawajui nini maana ya bima mfano unakuta wana viwanda lakini mpaka sasa havijakatiwa bima wakati ni kitu pekee na cha msingi katika usalama wa mali zao”alisema JOAN KIRWAY

Naye afisa ushirika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe, EXVERY SAPALI amesema sheria namba sita ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013 haina makali sana ya kuwabana wabadhirifu wa mali ndio maana wengi wamekuwa wakikiuka utaratibu na sheria za ushirika.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )