Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, March 13, 2019

Wafikishwa Kizimbani kwa Meno ya Tembo ya Bilioni 1

juu
Wakazi wawili wa Chanika Kwa Zoo, Dar es Salaam, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za  kukutwa na vipande 47 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni moja.

Washtakiwa hao, Abdallah Hamis (30) na Adam Kawàmbwa (35), walipanda kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Rwezile.

Wakili wa Serikali, Candid Nasua alidai washtakiwa walitenda makosa hayo Februari 11, mwaka huu eneo la Chanika Kwa Zoo, Ilala Dar es Salaam.

Alidai kuwa katika shtaka la kwanza, washtakiwa hao walikutwa wakimiliki vipande 47 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh 1,081,357,500 mali ya Serikali bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama Pori nchini.

Ilidaiwa kwamba katika shtaka la pili washtakiwa walitakatisha fedha hizo wakati wakijua zimetokana na kosa la ujangili.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwakuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Wakili Nasua alidai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kesi iliahirishwa hadi Machi 25, mwaka huu itakapotajwa.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )