Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, April 12, 2019

Baba Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kuzaa na Binti yake wa Kumzaa

juu
Mkazi wa kijiji cha Mwanzamiso wilayani Misungwi  mkoa wa Mwanza, Jacob Shabani (30) amefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma ya kumuweka kinyumba mwanaye na kuzaa naye watoto wawili.

Akisoma hati ya mashataka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi, Erick Marley juzi, mwendesha mashitaka wa polisi, Ramsoney Salehe alidai mshtakiwa alimuweka kinyumba mwanaye wa kumzaa kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka jana.

Alidai kuwa mshitakiwa alimuweka kinyumba mwanaye huyo mwenye umri wa miaka 17 na kumzalisha watoto wawili na kwamba alikuwa akiishi nae chumba kimoja.

Mwendesha mashtaka huyo aliendelea kudai kuwa, kwa sasa amebaki mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na mwingine aliyekuwa na umri wa miaka mitatu alifariki dunia.

“Mtuhumiwa alibainika anaishi na mwanaye wa kike chumba kimoja na kulala nae kitanda kimoja na alikamatwa baada ya wananchi kutoa taarifa kuhusu tukio hilo,” alidai Salehe. Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana makosa hayo.

Upande wa mashtaka ulieleza kuwa upelelezi umekamilika.

Hakimu Marley aliahirisha shauri hilo hadi Aprili 23 kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa na mtuhumiwa alirudishwa rumande baada ya kukosa mdhamini.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )