Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, April 4, 2019

Godbless Lema Asimamishwa Kuhuduria Mikutano Mitatu Ya Bunge....Wabunge wa Upinzani Wasusa na Kutoka Nje

juu
Bunge limepitisha Azimio la kumzuia  Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge kwa kosa la kulidhalilisha Bunge kwa kusema “Bunge ni dhaifu” na alipoitwa kwenye kamati ya Bunge ya kinga haki na madaraka ya Bunge hakuonyesha kujutia kufanya kosa hilo

Akiwasilisha hoja hiyo Bungeni leo April 4, 2019  mwenyekiti wa kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka  amesema kuwa Mbunge huyo alipopewa nafasi ya kujitetea kwenye kamati alisema ahukumiwe tu kwani alichozungumza ni kweli.

Wakati azimio hilo linapitishwa wabunge wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA  wamesusia kikao hicho cha bunge  na kutoka nje.

Baada ya wabunge hao kutoka nje, Spika Ndugai ameagiza wasiruhusiwe  kurudi ndani ya ukumbi  wa bunge kwa siku nzima ya leo

ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )