Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, April 12, 2019

Mbunge aomba kutengwa bajeti ya kutosha uchaguzi Serikali za mitaa

juu
Mbunge wa Nanyamba(CCM), Abdallah Chikota ameiomba serikali kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa ili changamoto zilizojitokeza kipindi cha nyuma zisijitokeze tena.

Akichangia Hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kwa mwaka 2019/20, Chikota  amesema ni vyema Tamisemi ikatenga fedha za kutosha kwa ajili ya kugharamia uchaguzi huo.

”Tuna uzoefu kwenye chaguzi zilizopita zilitengwa fedha ndogo na halmashauri kuambiwa waongezee kiasi kilichobaki,”amesema.

Amefafanua kuwa Halmashauri nchini uwezo wake unafahamika hivyo wasipewe mzigo hivyo fedha zitengwe za kutosha ili uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa na kukamilika bila kuwepo dosari yoyote.

Akizungumzia kuhusu Wakala wa Barabara mijini na Vijijini(Tarura), Mbunge huyo amesema Tarura inafanya kazi kubwa na imeonyesha mafanikio lakini ina changamoto ya  uhaba wa fedha na watumishi.

”Walipewa watumishi wachache kutoka mamlaka za serikali za mitaa na kutengeneza pengo kwenye uhaba wa wahandisi nashauri ifisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na utumishi wa umma watoe kibali  ili Tarura wapate watumishi,”amesisitiza Chikota.

Pia, ameishauri ofisi ya Rais Tamisemi kutatua changamoto ya wakuu wa idara ambao wamekuwa na makaimu wengi kutokana na uwepo wa malalamiko mengi ambayo yanatolewa na wakurugenzi kwamba suala la upekuzi linachukua muda mrefu.

”Kwahiyo hili suala la upekuzi kama walivyosema wajumbe wengine tuliwekee mkakati ili ufanyike kwa muda mfupi na wenye sifa waweze kuteuliwa,”amesema Chikota.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )