Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, April 12, 2019

Mtulia Abanwa bungeni...Ni Baada ya Kudai Wabunge wa CHADEMA Wamepatikana kwa aibu

juu
Wabunge wa Chadema wamemcharukia Mbunge wa Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia kwa kutoa kauli yake kuwa baadhi ya wabunge wa chama hicho walipatikana kwa aibu.

Leo Ijumaa Aprili 12,2019 ziliibuka kelele nyingi ndani ya Bunge hilo, wakimtaka Mtulia kuthibitisha jambo hilo kama hawezi afute kauli yake.

Mtulia amekutana na maswahibu hayo kutokana na taarifa aliyoitoa wakati mbunge wa Viti maalumu (Chadema), Grace Kihwelu alipokuwa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara zilizo chini ya ofisi ya Rais (Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora).

Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko ameomba mwongozo wa Spika kwa kutumia kanuni ya 64 kuhusu utaratibu ambapo amemtaka Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kumweleza Mtulia athibitishe aibu gani wanayoifanya Chadema hata kupata ubunge.

"Mheshimiwa mwenyekiti, sisi sote humu ndani tunaingia kwa kupigiwa kura na wananchi na kufuata utaratibu, naomba mbunge atuambie aibu gani walifanya wabunge wa upande huu hata wakapata ubunge," amesema Matiko.

Wakati mbunge huyo akitoa taarifa yake, wabunge wengi walikuwa wakipiga kelele na baadhi kuzomea jambo lililowafanya wabunge wa CCM kusimama akiwemo Magreth Sitta waliokuwa wakimtaka Mtulia kufuta kauli yake.

Chenge alimpa nafasi Mtulia kuchagua kama anaweza kufuta kauli au anaweza kuthibitisha kauli yake lakini alichagua kuifuta.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )