Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, April 12, 2019

Polisi Afikishwa Mahakamani Kwa Utapeli wa Milioni 489

juu
Ofisa wa Polisi, Lidya Nguwa amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 22 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha  Sh 489.6 milioni.

Akisoma hati ya mashtaka leo,  Wakili wa Serikali, Easter Martine alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando kuwa, mshtakiwa amejipatia fedha kwa njia ya udanganyifu Sh 489.6 milioni kutoka kwa watu 22.

Ilidaiwa kati ya tarehe tofauti mwaka 2018 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa  alijipatia Sh15.3 milioni kutoka kwa Happy Mhando kwa nia ya kuwekeza kwenye vikoba huku akijua anatapeli kwa ajili ya matumizi yake binafsi.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kati ya Septemba, 2018 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa  alijipatia Sh13.2 milioni kutoka kwa Elicia Kisoma kwa nia ya kuwekeza kwenye vikoba huku akijua anatapeli kwa nia ya matumizi yake binafsi.

Shtaka la nane, ilidaiwa  katika tarehe tofauti mwaka 2018 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa  alijipatia Sh10.9 milioni kutoka kwa ACP Imelda Tweve kwa nia ya kuwekeza kwenye vikoba huku akijua anatapeli kwa nia ya matumizi yake binafsi.

Kagika shtaka la tisa, ilidaiwa katika tarehe tofauti mwaka 2018 jijini Dar es Salaam, alijipatia Sh67 milioni kutoka kwa ofisa wa polisi, Richard Minja kwa nia ya kuwekeza kwenye vikoba huku akijua anatapeli kwa nia ya matumizi yake binafsi.

Shtaka la 10, ilidaiwa kati ya tarehe tofauti mwaka 2018 akiwa jijini Dar es Salaam alijipatia Sh9.04 milioni kutoka kwa ACP, Sarah Komba kwa nia ya kuwekeza kwenye vikoba huku akijua anatapeli kwa nia ya matumizi yake binafsi.

Katika shtaka la 12, ilidaiwa katika tarehe tofauti mwaka 2018 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alijipatia Sh115.8 milioni kutoka kwa Henry Lwiza kwa nia ya kuwekeza kwenye vikoba huku akijua anatapeli kwa nia ya matumizi yake binafsi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana mashaka yote yanayomkabili.

Hakimu Mmbando alisema dhamana ipo wazi hivyo mshtakiwa anatakiwa kuwasilisha nusu ya fedha taslimu anazodaiwa kujipatia kwa njia ya udanganyifu au awasilishe hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya fedha hizo.

Alisema mshtakiwa pia anatakiwa awe na wadhamini wawili wanaotambulika wenye barua kutoka kwa mkurugenzi wa manispaa na vitambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho(Nida) watakaowasilisha hati ya nusu ya fedha ya mali isiyohamishika.

Mshtakiwa huyo ameshindwa kutimiza masharti hayo na amerudishwa rumande hadi shauri bilo litakapotajwa tena Aprili 24.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )