Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, April 12, 2019

Rais Magufuli kuzindua mji wa Serikali Dodoma Kesho

juu
Rais wa Tanzania, John Magufuli kesho Jumamosi Aprili 13, 2019 anatarajiwa kuzindua mji wa Serikali uliojengwa katika eneo la Mtumba jijini hapa.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge leo Ijumaa Aprili 12, 2019 jijini Dodoma amewaambia waandishi wa habari kuwa mchakato wa ujenzi wa mji wa Serikali ulianza Novemba 2, 2018 huku ukigharimu kiasi cha Sh23 bilioni kwa wizara zote pamoja na ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali.

Pia amesema kiasi cha Sh2.27 bilioni kilitolewa na wizara ya fedha na mipango kwa ajili malipo ya fidia kwenye maeneo ya Mtumba, Mahoma pamoja na Makulu yaliyopo katika mji wa Serikali.

“Fedha zote hizo zimetolewa na wizara ya fedha na mipango kwa ajili ya mji wa Serikali lengo likiwa ni kutekeleza juhudi za Serikali ya awamu ya tano za kuhamishia Serikali Dodoma katika kipindi cha muda mfupi wa uongozi wake,” amesema Dk Mahenge.

Dk Mahenge amesema hadi kufikia Machi 26 mwaka huu majengo 20 yalikuwa yamekamilika ambapo majengo ya wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano yanatarajiwa kukamilika April 14, 2019.

Hata hivyo ujenzi wa mradi wa mji wa Serikali ulizalisha ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 1,288 kuanzia hatua ya awali hadi sasa kwa wakazi wa Dodoma.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )