Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, April 19, 2019

Tume Ya Taifa Uchaguzi Yakusudia Kutoa Elimu Kwa Watu Wenye Ulemavu Kabla ya Uchaguzi mkuu 2020

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020,Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu  inatarajia kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu  nchi nzima namna ya kushiriki kupiga kura .
 
Pia Tume hiyo itaandaa mfumo wa karatasi Nundu kupata   fursa  kwa walemavu kuchagua viongozi wa ngazi zote tofauti  na chaguzi za nyuma ambapo walipata fursa kupitia mfumo huo kuchagua Rais Pekee.
 
Hayo yamesemwa jana April 18 ,bungeni jijini Dodoma na Naibu waziri wa Kazi,Ajira ,vijana na watu wenye Ulemavu Mhe.Antony Mavunde wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti Maalum ,Suzan Chogisasi Mgonokulima aliyehoji serikali imetoa elimu kwa kiasi gani kwa watu wasioona ili waweze kupata mwongozo mzuri pindi wanapofika kwenye vituo vya kupigia kura.
 
Katika majibu yake,Mhe,Mavunde amesema tume ya taifa ya Taifa ya uchaguzi ina mkakati wa kutoa elimu kwa walemavu na kuongeza kuwa mwaka 2020 walemavu wote wa macho  watapata nafasi ya kuchagua viongozi wa ngazi zote kupitia mfumo wa maalum wa karatasi nundu tofauti ilivyokuwa mwaka 2015 ambapo walipata nafasi ya kuchagua nafasi ya Urais pekee kupitia mfumo huo.

Ikumbukwe kuwa , kifungu cha  61 ,kifungu kidogo cha 3[b] cha sheria ya Taifa ya uchaguzi  sura ya 343  na kifungu cha 62 [h]cha sheria za uchaguzi  serikali za mitaa sura ya 292 kinafafanua kuwa ikiwa mpiga kura ni mlemavu wa macho au mlemavu wa viungo ,mikono au hajui kusoma na kuandika  anaweza kumchagua mtu anayemwamini  ili aweze kumsaidia  kupiga kura.
 
Hivyo mtu huyo anapaswa kuwa msimamizi mkuu,msaidizi wa kituo cha kupigia kura au awe wakala wa chama cha siasa.
 
Vilevile kanuni ya 53 ya kanuni za uchaguzi wa wabunge na Rais mwaka 2015 na kanuni ya 46 ya chaguzi za serikali za mitaa ,madiwani  imeelekeza iwapo mpiga kura ni mlemavu wa macho ataomba karatasi za Nukta nundu ili aweze kupiga kura na msimamizi atawajibika kumpatia .
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )