Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, April 25, 2019

Waziri Ummy Azitaka Halmashauri Kote Nchini Kuhakikisha Zinatenga Bajeti Maalum Kwa Ajili Ya Kutekeleza Mikakati Ya Kupambana Na Malaria

juu
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Ikiwa leo ni   Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo huadhimishwa April 25 ya kila mwaka  , Waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia , wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu  amesema kuwa ni wajibu wa kila halmashauri kuhakikisha kuwa wanatenga bajeti  maalumu  kwa ajili ya kutekeleza mikakati mbalimbali ya kupamba na malaria.

Waziri Ummy ametoa rai hiyo   April 24 ,jijini  Dodoma alipotembelea  katika kituo cha afya cha Makole Mkoani  Dodoma   kwa ajili ya  kukabidhi vyandarua vyenye dawa viuatilifu katika kutekeleza   adhma ya serikali ya kuwakinga akina mama wajawazito pamoja watoto dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Aidha, waziri  ummy amesema kuwa kati magonjwa ambayo yanaongoza  kuua watanzania ni ugonjwa wa malaria lakini  habari njema ni kwamba toka serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  aingie madarakani wameweza kutekeleza mikakati mbalimbali ya kutokomeza  malaria nchini Tanzania.

Mbali na hilo amesema kuwa akina mama wajawazito wanatakiwa kuhudhuria kliniki mara tu wanapo gundua kuwa ni wajawazito   huku akibainisha  mikakati mbalimbali wanayo itekeleza kama serikali kupitia wizara ya afya kwaajili ya kutokomeza malaria .

Kwa upande wake Fransis Bujiku   ambaye pia Kaimu Mganga  Mkuu wa Mkoa  lakini pia anaratibu kitendo cha udhibiti wa Malaria mkoa wa Dodoma  , amesema kuwa kwa mwaka 2015 kulikuwa na kiwango cha maambukizi kwa asilimia moja  na kwa  kiwango hicho wameweza kukishusha mpaka asilimia 0.6 hivyo ni mafaniko makubwa.

Akizungumza kwa niaba  ya akina mama waliopokea msaada huo , mmoja wa  akina mama hao, Amina Alphonce ameishukuru wizara ya afya kwa kuwapatia vyandarua hivyo kwani vitawasaidia katika kujikinga na ugonjwa wa malaria pamoja na kutoa ushauri kwa  wakina  mama wenzake kuwa na tabia ya kuhudhuria  vituo vya afya.

Kauli mbiu ya  Maadhimisho ya Malaria mwaka huu 2019 ni  ‘’ Zero Malaria inaanza na Mimi’’.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )