Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, May 24, 2019

Kigwangallah: Ni Marufuku Kusafirisha Wanyama Hai Nje ya Nchi

juu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema hakuna viumbe hai watakaosafirishwa nje ya Tanzania, hata iwe kunguni au chawa.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Mei 24, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya wizara yake mwaka 2019/2020, kubainisha kuwa kitendo cha kusafirisha wanyama hakiungi mkono hivyo asingependa ifanyike akiwa katika wadhifa huo.

”Biashara ya wanyamapori hai haitafanyika nikiwa kama Waziri wa Maliasili na Utalii kwakuwa suala hilo lilishafungwa.

“Wizara imeamua kufunga mlango wa biashara hii, hata awe chawa au kunguni, atakayetaka kufuga afuge ili watanzania waende kwenye Zoo yake kuwatazama wanyama hao,” amesema Kingwangalla.

Ameongeza kuwa kuhusu suala la vipepeo kusafirishwa kwenda nje ya nchi wananchi ambao walikuwa wamechukuliwa vipepeo vyao ili viakuzwe watarudishiwa fedha zao na serikali.

Wakati huo huo Waziri huyo amesema kuwa Rais John Magufuli ameridhia hifadhi tatu mpya kuingizwa katika orodha ya Hifadhi za Taifa.

“Hapa nina hati kutoka kwa Rais, ameridhia hifadhi mpya tatu kuingia katika orodha ya hifadhi za taifa,” amesema Kigwangalla

Amezitaja hifadhi hizo mpya kuwa ni hifadhi ya Burigi, Chato, hifadhi ya Rumanyika, Karagwe na Ibanda, Kyerwa.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )