Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, May 24, 2019

Rais Magufuli Aondoka Nchini Kuelekea Afrika Kusinj

juu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Mei, 2019 ameondoka nchini kwenda Afrika ya Kusini ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa.

Katika safari hiyo Rais Magufuli ameongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Philip Mangula na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.

Wakizungumza kabla ya kuondoka Rais Mstaafu Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa CCM Mangula wamesema Tanzania na Afrika ya Kusini zina uhusiano mkubwa na wa kihistoria na kwamba Serikali na chama zina kila sababu ya kudumisha uhusiano na ushirikiano huo.

Viongozi hao wameondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Afrika ya Kusini, Mhe. Rais Magufuli atafanya Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Namibia ambako pia atazindua mtaa uliopewa jina la Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kutambua mchango mkubwa alioutoa katika ukombozi wa Taifa hilo.

chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )