Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, May 29, 2019

Serikali Yaanza Utekelezaji Wa Mkakati Wa Mpango Miji Ambapo Maeneo Yaliyoiva Kuwa Miji Yafikia 455 Hapa Nchini.

juu
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imeanza utelekelezaji   wa mkakati wa kupanga miji yote nchini  ambapo maeneo yaliyofikia kuwa miji hadi sasa ni Zaidi ya 455. 

Hayo yamesemwa leo Mei 29,2019 na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi wakati akijibu swali la Mbunge wa Kasulu mjini Daniel Nicodemus Nsanzugwako  aliyehoji kwanini serikali isije na mkakati endelevu  wa kupanga miji  yote iliyotangazwa kwenye gazeti la serikali. 

Katika majibu yake,Waziri Lukuvi amesema serikali imeanza utekelezaji wa mkakati wa kupanga miji yote  ambayo imetangazwa  kwenye gazeti la Serikali  kwa kuandaa mipango kabambe ya majiji,manispaa,na miji. 

Aidha,Serikali imeainisha maeneo yote ambayo yameiva kuendelezwa kimji  kwa ajili ya kuyatangaza kwenye gazeti la serikali  kuwa maeneo mipango ambayo ni Zaidi ya maeneo 455 nchini.

Hata hivyo,Waziri Lukuvi amesema kwa mujibu wa kifungu Na.7[1] na 5 cha Sheria ya Mipango miji  Na.8 ya mwaka 2007,jukumu la kupanga na kupima miji ni la mamlaka za upangaji ambazo ni Halmashauri za majiji,manispaa,miji ,na mamlaka za miji midogo. 

Waziri Lukuvi amebainisha,Serikali imeendelea kuzisaidia halmashauri  kupanga na kupima miji  yao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo  ambapo mwaka 2018/2019 serikali kupitia Wizara  imetoa Jumla ya Shilingi Bilioni 6.4 kwa halmashauri 29 nchini  kwa ajili ya upangaji,upimaji na umilikishaji wa  ardhi .

Pia imewezesha uandaaji wa mipango kabambe ya miji 18  kupitia program ya kuzijengea uwezo  mamlaka za miji [Urban Government Strengthening Program-ULGSP] Chini ya Ofisi ya Rais –TAMISEMI.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )