Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, May 24, 2019

Serikali Yasema Itawafuta Kazi Viongozi Wataoshindwa Kuendana Na Kasi Ya Serikali Ya Awamu Ya Tano.

juu
Na Salvatory Ntandu
Serikali kupitia Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma imesema itachukua hatua kali kwa Viongozi wa Umma ambao watabainika kukiuka sheria ya Maadili ya viongozi wa Umma kwa makusudi kwa kujinufaisha wao binafsi na kukwamisha malengo ya serikali ya awamu ya tano.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu katibu Msaidizi wa ofisi sekretarieti ya maadili ya umma kada ya Magharibi Tabora GERAD MWAITEBELE katika hafla ya siku mmoja ya mafunzo ya kwa viongozi wa Umma iliyojumisha viongozi wote wa Umma katika Halmashauri ya Mji wa kahama mkoani Shinyanga.

Amesema baadhia ya viongozi wa umma wanajisahau na kujikuta wanaingia katika vishawishi ikiwemo kupokea zawadi ambazo husababisha kushindwa kufanya maamuzi katika nafasi walizopewa na serikali hali ambayo inachangia kurudisha nyuma maendeleo na kuisababishia hasara serikali.

Amefafanua kuwa kwa sasa Ofisi yake inaendelea Kutoa elimu kwa viongozi wa umma ili kuwakumbusha majukumu yao,sheria,matamko na kanuni zilizowekwa na serikali katika kuhakikisha kila kiongozi wa umma anafanya kazi yake kwa usahihi bila kuvunja sheria.

Kwa upande wake Katibu tawala wa wilaya ya kahama Timoth Ndanya ambaye alikuwa mgeni rasm katika mafunzo hayo amewataka Viongozi wa umma kucha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wajitathimini kama wanafaa katika nafasi walizopewa jambo ambalo litaweza kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za Umma.

Naye mkuu wa Polisi Kahama (SSP) Sophia Jongo amesema viongozi wengi waumma wanashitakiwa kwa kukiuka sheria hiyo  na kuiomba serikali iweke mtaala wa sheria hii kwa gazi zote za elimu hapa nchini.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )