Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, July 28, 2019

Lugola Amtumbua Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO), Charles Bukombe

juu
 Na Felix Mwagara, MOHA-Malinyi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuondoa madarakani Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO), Charles Bukombe kwa kosa la kuyapuuza maagizo yake na kuyaita ya kisiasa.

Licha ya kumuondoa katika nafasi hiyo, Waziri Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake, kumchukulia hatua kali za kinidhamu RTO huyo ili iwe fundisho kwa matrafiki hao wa mikoa nchini.

Lugola amesema RTO huyo ameshuhudia katika video ambayo ilikua inasambaa mitandaoni akiwa katika mkutano jijini Arusha, akipinga maagizo yake na kuyaita ya kisiasa na pia kutokuyatekeleza.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Mji wa Malinyi, Mkoani Morogoro, leo, Lugola amesema yeye hatoi maagizo ya kisiasa bali anatoa maagizo yatakayomsaidia Rais kazi zake kwa wananchi wanyonge wanaopambana na umaskini na ajira.

“Namuagiza katibu Mkuu achukue hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumuondoa u-RTO afanye shughuli zingine za kipolisi, na maRTO ambao mkono wangu haujafika kwenu, na wengine nimeanza kuwaona hamsimamii vizuri maagizo yangu, wapo ambao wanaendelea na uonevu, wapo baadhi ya askari wanaendelea kuchukua rushwa barabarani,” alisema Lugola.

Pia Waziri Lugola ametoa onyo kali kwa MaRTO Mikoa ya Morogoro na Mara akiwataka wachukue fursa ya kujitathimini katika utendaji wao kabla hajawachukulia hatua.

“Wapo baadhi ya askari waonevu, wanaendelea kuchukua rushwa, wajitathimini, katika utendaji wao kabla sijawachukulia hatua kali za kinidhamu,” alisema Lugola.

Lugola katika hotuba zake katika mikutano yake mbalimbali alisema Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na haitaki kumnyanyasa mwananchi yeyote kupitia makosa ya trafiki wasiokuwa waaminifu.

Lugola alitoa maagizo kwa Jeshi la Polisi nchini, kuwa bodaboda zinazotakiwa kuwepo kituo cha polisi ni zile zilizopo katika makundi matatu ambayo ni Bodaboda zilizohusika kwenye uhalifu, zilizotelekezwa au zilizookotwa na zilizohusika katika ajali.
 
“Bodaboida hizo ndizo zinapaswa kuwepo vituoni, lakini kuziweka bodaboda ambazo hazipo katika makundi hayo, napiga marufuku na hii nataka Polisi nchi nzima munielewe,” alisema Lugola.

Pia Lugola aliwataka waendesha bodaboda mjini Malinyi na Tanzania kwa ujumla wafuate sheria za usalama barabarani zikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa.

Pia Waziri Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya askari Polisi hapa nchini kukamata pikipiki wakiwa hawana sare za Jeshi, anasema kwa kufanya hilo kunaleta kero kwa madereva na pia anayekamatwa anaweza akadhaniwa kuwa ni jambazi.

Lugola anaendelea na ziara yake mkoani Morogoro, na
anatarajia kumaliza ziara hiyo Wilaya ya Ulanga Mkoa humo
Julai 29, 2019.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )