Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, July 22, 2019

Mawakala wawili wa ununuzi wa kahawa wanasakwa mkoani kagera kutokana na kupinga maagiuzo ya serikali.

NA AVITUS BENEDICTO KYARUZI,KAGERA
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameagiza kukamatwa mara moja kwa Mawakala wawili wa Kampuni binafsi wanaopita vijijini katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa kuwapotosha na kuwalaghai wakulima wa kahawa wasikubaliane na mfumo wa Serikali wa kukusanya kahawa katika vyama vya msingi na kuiuza kwa mfumo wa ushirika ulionzishwa na Serikali.
 
Mkuu wa Mkoa Gaguti ametoa maelekezo hayo july21 katika mkutano wa viongozi wa Vyama vya Msingi, Watendaji wa Kata na Viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika cha KDCU Limited Wilayani Karagwe mara baada ya kukagua viwanda vitatu vya kukoboa kahawa vya Karim Amri, ASU Company Limited na KDCU Limited kuona namna vinavyoendelea kuchakata kahawa.
 
Mkuu wa mkoa  Gaguti amesema kuwa maelekezo ya Serikali yapo wazi kuwa kama kuna mfanyabiashara yeyote anataka kununua kahawa awasiliane na ofisi yake lakini awe na bei inayomnufaisha mkulima. 
 
Kuhusu bei kwamba wakulima wanapunjwa Mkuu wa Mkoa Gaguti aliitolea ufafanuzi kuwa mpaka mkulima analipwa malipo ya kwanza tayari Vyama Vikuu vya Ushirika vinakuwa vimeondoa gharama za uchakataji kiasi cha shilingi 600 na kupelekea kilo moja kufika hadi 1700/= lakini bado bei katika soko la dunia ikitangazwa mkulima anaongezewa fedha nyingine wakati makato yote ya Serikali na gharama za uchakataji zinakuwa zimelipwa tayari.
 
Aidha, Mzee Thomas Kasimbazi mkulima kutoka Chama cha Msingi Nyabwegira Kata Ndama aliiomba Serikali inapokuwa na mipango mizuri iwashirikihe wananchi ili waweze kuelewa hasa suala la mkulima kulipiwa benki ambapo mzee Kasimbazi alisema kuwa wazee wengi hawajui na hawaelewi kwanini wanalipiwa Benki baada ya kukusanya kahawa yao katika Vyama vya Msingi ambapo wakipata elimu wapo tayari kutoa ushirikianao kwani Serikali inalenga kulinda fedha zao ziwafikie walengwa moja kwa moja.

Akifafanua Mkuu wa MkoaGaguti alisema kuwa tayari elimu inaendelea kutolewa chini ya uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ikishirikiana na mitandao ya simu, TCRA, na Benki zinazohusika katika malipo wanapita kwa wakulima na kuwaelimisha faida za kulipiwa benki pia Mkuu wa Mkoa Gaguti aliagiza Wakuu wa Wilaya kubaini maeneo yenye changamoto ya mitandao na wakulima wenye fedha chini ya Tshs 100,000/= kupelekewa fedha zao taslimu bila kuzipitisha benki.

Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera vya KCU 1990 LTD na KDCU LTD tayari vimekusanya kahawa kilo milioni 8.5 sawa na asilimia 20% ya malengo ya ukusanyaji katika msimu huu wa mwaka 2019/20 na jumla ya shilingi bilioni 6.2 tayari zimelipwa kwa wakulima aidha, KDCU LTD tayari kimekusanya kahawa ya maganda kilo milioni 5.8 na shilingi bilioni 5.3 zimelipwa kwa wakulima sawa na asilimia 15% ya matarajio ya makusanyo.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )