Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, July 5, 2019

SBL yafanya ‘hafla kuipongeza Taifa Stars’ baada ya kurejea kutoka AFCON

juu
Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa bia nchini Tanzania, Serengeti Breweries Limited (SBL), imeandaa hafla ya chakula cha mchana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuipongeza Timu ya Taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) baada ya kurejea kutoka nchini Misri ilipokwenda kushiriki kwenye fainali zinazoendelea za kombe la mataifa barani Afrika (AFCON 2019).

Licha ya kupoteza mechi zake tatu za hatua ya makundi na hivyo kushindwa kusonga mbele kwenye hatua zinazofuata za mashindano hayo, Taifa Stars inayodhaminiwa na SBL inastahili pongezi kwa kuweza kufuzu kushiriki fainali hizo za mashindano makubwa ya mpira wa miguu barani Afrika baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa takribani miongo minne.

Akiongea kwenye hafla hiyo ambayo imefanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza amewashukuru wachezaji na viongozi wa Taifa Stars kwa kutimiza ndoto ya Tanzania kushiriki katika fainali za AFCON. “Kitendo cha kuweza kufuzu kushiriki fainali za mashindano haya ni hatua moja kubwa mbele ikizingatiwa tumejaribu mara kadhaa bila kufanikiwa, hivyo basi kwa hatua ambayo tumeweza kufika, kila mmoja aliyeshiriki kuifikisha hapa timu anastahili pongezi”. Alisema Anitha huku akiongeza kuwa kiwango walichoonyesha Taifa Stars kilionekana ‘kuimarika zaidi’ licha ya matokeo kutoridhisha.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Kidao Wilfred ameishukuru SBL kwa mchango wake mkubwa kwenye timu ya taifa na kuongeza kuwa udhamini wa SBL kwa Taifa Stars umekuwa na mchango kubwa katika kuiwezesha timu kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali yanayoikabili.

“Tutakutana na benchi la ufundi ili kufanya tathimini juu ya ushiriki wa timu yetu kwenye fainali za AFCON 2019, baada ya hapo tutakuja na mkakati kwa ajili ya mashindano yaliyoko mbele yetu ya kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN)”. Alisema Kidao huku akidokeza kuwa timu imepata ‘funzo kubwa’ kule Cairo.

Taifa Stars inayodhaminiwa na SBL imeweza kushiriki katika fainali za AFCON 2019 kwa mara ya kwanza tangu mara ya wisho ilipofanikiwa kufuzu kucheza fainali hizo takribani miaka 39 iliyopita. Stars ilipangwa kwenye kundi C ambalo lilijumuisha magwiji wawili wa soka barani Afrika (Senegal na Algeria) pamoja na Kenya.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )