Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, July 12, 2019

Wizara Ya Fedha Na Mipango Yatwaa Tuzo Mbili Maonesho Ya Kimataifa Ya Biashara Dare Sa Salaam

juu
Na Mwandishi wetu, WFM, Dar es Salaam
WIZARA ya Fedha na Mipango, imetwaa tuzo mbili kwa mpigo kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayofikia kilele Jumamosi Julai 13, 2019.

Katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonesho hayo kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa (Ceremonial dome) , Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alikabidhi tuzo hizo moja baada ya nyingine, kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja.

Akizungumzia tuzo hizo Bw. Mwaipaja alisema moja ni ya mshindi wa pili katika ubunifu wa mfumo wa ukusanyaji maduhuli ya serikali (GePG) ambao umerahisisha mfumo wa malipo kwa wananchi, wakiwemo pia wafanyabiashara, na wawekezaji.

Aidha, Taasisi mbili za Wizara ya Fedha na Mipango, ikiwemo Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), zimetwaa tuzo ya mshindi wa Tatu katika utoaji wa Elimu bora ya Juu na Usimamizi makini wa wataalamu wa Ununuzi na Ugavi.

Maonesho hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere maarufu Sabasaba, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, yamebeba kauli mbiu isemayo "Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda."
 
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )