Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, August 20, 2019

Aliyejifanya ofisa wa Jeshi la Polisi na la Kujenga Taifa (JKT) Apandishwa kizimbani

adv1
David Ramadhani Iddy (33) mkazi wa Tabata Segerea   amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kinondoni  kwa kosa la kujifanya ofisa wa Jeshi la Polisi na la Kujenga Taifa (JKT).

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Joyce Moshi na Mwendesha Mashtaka wa Serikali ASP Hamisi alidai julai 19, 2019 eneo la  Makao Makuu JKT Mlalakua wilayani Kinondoni Dar es salaam kwa nia ya udanganyifu alijitambulisha kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi kwa cheo cha MP.

Katika shtaka la pili julai 19, 2019 eneo la Makao Makuu ya JKT Mlalakua wilayani Kinondoni Dar es salaam alikutwa na vifaa vya Umma kinyume na sheria kama sare kamili za askari, sare za askari za kijani, beji na vyombo vya askari, kofia ya askari, kofia ya askari wa usalama wa barabarani, sare za viatu za askari , buti, pingu na redio call.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka mbele ya Mahakama na ASP Hamisi alisema upelelezi wa shauri hili unaendelea tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Moshi alisema dhamana yake ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye kusaini bondi ya sh 2,000,000 kila mmoja, barua za utambulisho na nakala ya vitambulisho.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapo kuja kusomwa tena septemba 2 mwaka huu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )