Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, August 17, 2019

PICHA: Marais 11, Makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu Wahudhuri Mkutano wa SADC Tanzania

adv1
Marais wa nchi 11 wamehudhuria mkutano wa kilele wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) unaofanyika jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Agosti 17, 2019 na kesho.

Mkutano huo umeanza saa 3:49 asubuhi na kuhudhuriwa na marais na mawaziri kutoka nchi wanachama, marais wastaafu, viongozi na washiriki mbalimbali.

Marais hao ni John Magufuli (Tanzania),  Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini), Azali Assoumani (Comoro),  Danny Faure (Shelisheli),  Joao Manuel Goncalves (Angola).

Wengine ni Edgar Lungu (Zambia), Felix Tshisekedi (DRC),  Andry Rajoelina (Madagascar), Emerson Mnangagwa (Zimbabwe), Filipe Nyusi (Msumbiji) na Dk Hage Geingob (Namibia).

Nchi  ya Eswatin imewakilishwa na waziri mkuu,  Ambrose Dlamini;  Lesotho pia imewakilishwa na waziri mkuu, Motsahai Thabane  huku Malawi ikiwakilishwa na makamu wa rais sambamba na Botswana na Mauritius zilizotuma wawakilishi.

Marais wastaafu wa Tanzania ambao wamehudhuria mkutano huo ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye ni Rais ww Serikali ya Awamu ya Pili,Benjamin Mkapa ambaye ni Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu,Jakaka Kikwete aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne na kwa upande wa Zanziabar Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Amani Karume.

Mbali ya wastaafu hao kuwemo kwenye mkutano huo ambao pia wametambulishwa kwa wageni mbalimbali kutoka nchi 15 za jumuiya hiyo,pia viongozi wengine wa Serikali ya Tanzania waliohudhuria ni Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Balozi John Kijazi,mawaziri, viongozi wa ngazi mbalimbali wastaafu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda.Pia wamehudhuria watu mashuri wa ndani na nje ya Tanzania.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )