Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, November 24, 2019

Radi Yaua Watatu Rukwa

juu
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa, Justine Matejo, amethibitisha kutokea kwa matukio mawili ya vifo ambavyo vimesabibishwa kwa mvumo wa radi, hali iliyopelekea watu watatu kufariki Dunia.

RPC Rukwa amesema, wamepokea taarifa hizo za matukio mawili tofauti ambalo moja lilitokea Novemba 23 saa 8:30 mchana, na lingine ni Novemba 19.

"Ni kweli kuna taarifa ambazo tumezipata kwamba huko maeneo ya Namanyele kuna kijiji kinaitwa Mwai, kuna watu wawili wamepigwa radi ambao walikuwa wamejihifadhi chini ya mti, hivyo radi ikapiga mti na watu hao wakapoteza maisha, watu hao ni Japhet Gerrald (25) na mtoto Peter Richard (8)" amesema

"Kuna tukio lingine ambao ni la muda lilitokea Novemba 19, maeneo ya kijiji cha Lahela Mume na Mke ambao walikuwa wamelala, kwa bahati mbaya radi ilipiga ila aliyefariki alikuwa ni Mke" ameongeza

Aidha RPC Rukwa ametoa rai kwa wakazi wa mkoani humo kwa kuchukua tahadhari kuwa wasikae katika miti kwa sababu inakuwa ni tatizo.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )