Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, November 5, 2019

Rais Xi Jinping wa China Aimwagia Sifa Tanzania....Korosho, Madini ya Tanzanite Yamvutia Zaidi

adv1
Maonesho ya pili ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa China yamefunguliwa leo mjini Shanghai, China. Rais Xi Jinping wa China amehutubia ufunguzi huo.

Maonesho hayo yenye kauli mbiu ya "zama mpya, kunufaika kwa pamoja na mustakabali wa pamoja" yameshirikisha zaidi ya makampuni 3,000 kutoka nchi na sehemu 150 za mabara matano duniani.

Katika hafla hiyo viongozi wa Mataifa 64 walihudhuria akiwemo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Mawaziri Wakuu wa Jamaica; Serbia na Greece huku ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa. ‪

Aidha baada ya kufungua maonesho hayo Rais wa China ametembelea Mabanda ya nchi (5) yakiwemo mabanda ya Ufaransa; Ugiriki; Serbia; Jamaica na Tanzania.

Katika ziara ya kutembelea Banda la Tanzania Rais Xi Jinping alifuatana na Waziri Mkuu wa Jamaica; Greece na Serbia na kupokelewa na Waziri Bashungwa.
 
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, alitoa maelezo juu ya bidhaa mbalimbali za kilimo na madini zinazopatikana nchini Tanzania na vivutio vya utalii. Aidha, Balozi Kairuki aliwasilisha salaam za Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli kwa Rais wa China.

Kwa upande wake Rais wa China ameipongeza Tanzania kwa kushiriki katika maonesho ya pili ya Kimataifa ya Bidhaa za Nje na ametuma salaam za pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na China.

Rais Xi alivutiwa zaidi na bidhaa ya korosho za Tanzania na madini ya Tanzanite ambapo alitaka kufahamu zaidi juu ya upatikanaji wa bidhaa hizo katika soko la China.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )