Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, November 8, 2019

Waziri Kangi Lugola amuagiza IGP Simon Sirro Kumchukulia Hatua Mbunge wa CHADEMA Kwa Kumtimua Mpangaji Wake

adv1
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Kangi Lugola amemuagiza IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mbunge Sophia Mwakagenda (CHADEMA), na wengine wanaotoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani

Mbunge huyo amesema amemuondoa mpangaji (Polisi) kwenye nyumba yake, kwa sababu haoni haja ya kushirikiana nae.
 
“Mimi Sophia Mwakagenda sina mtendaji wala sijui kiongozi gani niishipo nitakaefanya nae kazi mpaka muweke mambo yenu sawa, pia leo namtoa kwenye nyumba yangu mpangaji wangu ambaye ni askari polisi akakae huko anakolipwa mshahara, nyumba ni yangu,” alisema Sophia.


Akijibu kauli hiyo Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Kangi Lugola amesema;“Jeshi la Polisi Tanzania tumekwishajipanga kuhakikisha amani inakuwepo kuanzia urejeshwaji wa fomu, rufaa, kampeni mpaka uchaguzi wa serikali za mitaa na matokeo. Hakuna Mtanzania yoyote, kikundi ama chama cha siasa kitakachofanya fujo ama kuharibu mali watu wakati wa uchaguzi.

“Nina taarifa chama kimoja kimejiondoa kwenye uchaguzi, ni imani yangu kwamba chama hicho kinaweza kuwa na mpango wa kuvuruga uchaguzi. Ninawaambia kwamba, hakuna chama chochote cha siasa kitakachovuruga uchaguzi, tutatumia nguvu yoyote kuhakikisha hakuna uvunjifu wa amani.

“Kuna viashiria vya uvunjifu wa amani vimeanza kujitokeza kuanzia humu Bungeni kwa kuwafukuza wapangaji, nawasishangae tukianza kuchukua hatua,. Tutaanzia hapa Bungeni kuchukua hatua.

“Namuelekeza IGP Sirro kuanza kuchukua hatua kuanzia Mbozi na kwa Mbunge huyu (Sophia Mwakagenda) ambaye ameanza kuonyesha viashiria vya uvunjishu wa amani. Wasiijaribu serikali ya awamu ya Tano, tuko vizuri sana, kiberiti kimejaa njiti, wakitikisa kitawaka,” amesema Lugola.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )