Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, December 20, 2019

Jeshi la Polisi Lasema Linamshikilia Tito Magoti Na Wenzake Watatu kwa mahojiano

adv1
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linamshikilia ofisa programu wa kituo cha sheria  na haki za Binadamu (LHRC), Tito  Magoti kwa mahojiano .

"Tunamshikilia Tito Magoti (26), Mkazi wa Ubungo Kibo, Afisa Programu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ( LHRC ) pamoja na Watu wengine watatu kwa uchunguzi na mahojiano kwa tuhuma za makosa ya jinai ”- Amesema Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Amesema Magoti na wenzake amekamatwa na Polisi  leo Ijumaa asubuhi maeneo ya Mwenge na wote kwa pamoja  wanaendelea kuhojiwa kwa tuhuma za makosa ya jinai.
 

“Tito Magoti hakutekwa bali amekamatwa na Polisi leo saa tano asubuhi maeneo ya Mwenge na yupo katika mikono salama, yeye na wenzake watatu wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa Mahakamani baada ya kukamilisha uchunguzi na mahojiano”amesema Mambosasa
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )