Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, December 22, 2019

Liverpool Yabeba Taji La Klabu Bingwa Duniani Kwa Mara Ya Kwanza

Liverpool wameibuka mabingwa wa kombe la Klabu Bingwa wa Dunia, baada ya kuifunga Flamengo ya nchini Brazil bao 1:0 katika mchezo wa fainali.

Roberto Firmino, mshambuliaji wa Liverpool ndo aliyefunga bao pekee la ushindi mbele ya timu ya Flamengo kwenye mchezo wa fainali ya kombe la klabu bingwa duniani.

Firmino alifunga bao hilo ndani ya dakika za nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika bila timu hizo kuonyeshana ubabe kwenye fainali hiyo ya kibabe.


Ushindi huo unaifanya Liverpool iliyo chini ya Jurgen Klopp kutwaa taji hilo la dunia kwa mara ya kwanza.


Liverpool imekua timu ya pili kutoka England kushinda ubingwa Wa Dunia kwa ngazi ya vilabu baada ya Manchester United kufanya hivyo mwaka 2008.
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )