Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, December 20, 2019

Muuguzi anayetuhumiwa kubaka Mjamzito asimamishwa kazi

juu
Na Rayson Mwaisemba WAMJW- Katavi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo ameliagiza Baraza la Uuguzi na Ukunga kumsimamisha kazi muuguzi anayetuhumiwa kumbaka mama mjamzito katika kituo cha Afya Mamba kilichopo Kijiji cha Mamba Mkoani Katavi ili kupisha uchunguzi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akiongea na Wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Majalila Wilaya ya Mpanda, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na uboreshaji wa miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

“Naliagiza baraza la wauguzi na ukunga kusimamisha leseni ya muuguzi huyu wakati uchunguzi unafanyika “Amesema Waziri Ummy.

Aidha,amewataka watumishi  wote wa afya nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na viapo vya kazi zao.

“Na yeyote atakayefanya kazi kinyume na maadili,weledi na kiapo chake tutamchukulia hatua za nidhamu ikowemo kuwafutia leseni zao na kuwapeleka katika vyombo vya
dola”.Amesisitiza Waziri Ummy.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )