Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 12, 2019

Viongozi Wa Umma Nchini Watakiwa Kusimamia Sheria,kanuni,taratibu Na Miongozo Ya Utumishi

adv1
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Viongozi wa Umma nchini wametakiwa kusimamia  Sheria,kanuni,taratibu na miongozo ya utumishi ili kutekeleza adhima ya Serikali ya kuboresha utumishi wa Umma.

Kauli hiyo imetolewa   na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kepteni Mstaafu George Mkuchika wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya maadili na haki za bianadamu kitaifa jijini Dodoma ambapo amewataka watumishi wa Umma kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili.

“Tunaona Maadili ndio neno la Msingi,Miongoni Mwa jitihada za serikali ni kutunga sheria na kanuni mbalimbali zinazozingatia Maadili na Kanuni za utumishi wa umma,hivyo niwaase watumishi wa umma kuzingatia katika kufuata na kusimamia sheria  na Miongozo ya utumumishi kwa lengo la kuboresha utawala bora”amesema.

Aidha ,amesema baadhi ya taasisi za umma zimeanzisha mabaraza ya kushughulikia utawala bora lengo kuu ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora.

Katika hatua nyingine Kaptain Mkuchika amesema suala la mfumo wa Mtandao limekuwa na mchango mkubwa katika kuhakiki watumishi feki pamoja na uadiluifu wa matumizi ya fedha za umma.

Awali  akizungumza katika maadhimisho hayo ,Naibu Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mary Mwanjelwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika masuala ya uadilifiu na uzalendo hivyo kila mmoja anapaswa mambo yasiyofaa katika taifa.

“Sisi tunatakiwa kuwa mfano bora katika kusimamia uadilifu na utawala bora hivyo niwaase watumishi wa umma kuwa jambo la uadilifu ni jambo la muhimu sana

Kwa upande wake  Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma Jaji Nstaafu Haroid Nsekela ameelezea chimbuko la siku hiyo kuwa ni siku ya kimataifa ya kuzuia na kupambana na Rushwa ambayo huazimishwa Desemba 09 ya kila mwaka

Tangu mwaka 2017 maadhimisho ya siku ya maadili na haki za bianadamu kitaifa yamekuwa yakifanyika Jijini Dodoma kufuatia maamuzi ya Serikali kuhamishia makao makuu jijini hapa na kauli mbiu kwa mwaka huu ni “maadili katika utumishi wa Umma ni nguzo Muhimu katika kuimarisha utawala bora na Haki za Binadamu”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )