Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 8, 2020

Breaking News: Iran Yarusha Makombora Na Kupiga Kambi za Jeshi la Marekani Huko Iraq

Jeshi la Iran (IRGC) limerusha makombora ya balestiki na kupiga kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq, kama jibu la kuuawa  Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH.

Taarifa ya IRGC imesema kuwa, Iran imetoa jibu hilo kwa  Marekani alfajiri ya leo, ambapo imelenga uwanja wa ndege wa kijeshi wa Marekani wa Ain al-Assad katika mkoa wa al-Anbar, magharibi mwa Iraq.

Jeshi la Iran limeitaka Marekani iwaondoea wanajeshi wake wote katika nchi hiyo ya Kiarabu, likisisitiza kuwa halitatenganisha kati ya Marekani na Israel katika kujibu mapigo ya kuuawa  Jenerali  wao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad javad Zarif amezungumzia  kuhusu shambulizi  hilo la Iran katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuandika: "Iran imechukua hatua madhubuti ya kujihami kwa mujibu wa Sura ya 51 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa kulenga kambi ya jeshi ambayo ilitumiwa katika shambulizi la kioga dhidi ya raia na maafisa wetu wa ngazi za juu. Hatutaki kukuza mambo wala vita, lakini tutajihami dhidi ya uvamizi wowote."

Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imethibitisha habari hizo za kuvurumishwa makumi ya makombora ya balestiki kuelekea katika kambi  ya jeshi la Marekani nchini Iraq.


Rais Trump pamoja na kusema atatoa taarifa leo, ila kupitia ukurasa wa Twitter amesema: “Kila kitu kiko vizuri! Makombora yamerushwa kutoka Iran kwenda kwenye kambi mbili za jeshi zilizoko Iraq. Tathmini ya majeruhi na uharibifu inafanyika sasa. Tuna vifaa vyenye nguvu na tumejizatiti vizuri kijeshi kuliko nchi yeyote duniani.”
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )