Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 28, 2020

Ester Bulaya Ateuliwa Kuwa mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Akichukua Mikoba ya Tundu Lissu

Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe (Mb) amemteua Mbunge wa Bunda (Chadema), Ester Bulaya kuwa Mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni.Ester anakuwa mwanamke wa kwanza kutumikia nafasi hiyo, tangu CHADEMA   ianze kuongoza kambi hiyo.
 
Leo Jumanne Januari 28, 2020 Spika Job Ndugai amemtangaza Bulaya akibainisha kuwa amepokea jina hilo kutoka kwa kiongozi wa kambi hiyo bungeni, Freeman Mbowe.

Bulaya anachukua nafasi ya aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyevuliwa ubunge kwa madai ya kutoonekana bungeni bila taarifa yoyote.

Kabla ya uteuzi huo wa Bulaya, mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alikuwa anakaimu nafasi hiyo. Selasini alijiuzulu wiki iliyopita.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )