Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 28, 2020

Kesi Ya Kupinga Kutenguliwa Kwa CAG Prof. Assad Iliyofunguliwa na Zitto Kabwe Imeanza Kusikilizwa Leo Mahakama Kuu.

juu
Mahakama Kuu ya Tanzania masjala Kuu Dar imeanza kusikiliza kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuhusu utenguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG),Prof. Mussa Asaad na Kumteuliwa kwa Mrithi wake Charles Kichere

Kesi hiyo imeanza kutajwa mahakamani hapo leo Jumanne Januari 28, 2020  kwa ajili ya kuangalia taratibu za awali za mwenendo wa kesi hiyo ambazo ni pamoja na pande husika kukabidhiana nyaraka zinazohusu kesi hiyo, kabla ya kuendelea na hatua nyingine. 

Katika kesi hiyo, Zitto ambaye  anawakilishwa na wakili Nyaronyo Kicheere, anapinga Sheria ya Ukaguzi ya Taifa namba 11 ya mwaka 2008 inayoweka vipindi viwili vya mtu kushika wadhifa wa CAG.

Pia, anapinga uamuzi wa Profesa  Assad  kuondolewa katika wadhifa huo, akidai ameondolewa kabla ya muda wake wa utumishi kwa mujibu wa katiba. 


Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji watatu Jaji Lameck Mlacha (kiongozi wa jopo), Jaji  Benhajj Masoud na Jaji Juliana Masabo.

Waidaiwa ambao ni Rais, AG na CAG Kichere akiwakilishwa na jopo la mawakili wa Serikali wanne na Profesa Assad anawakilishwa na jopo la mawakili wawili linaoongozwa na Ambros Mkwera, wameomba muda wa siku 14 kuwasilisha majibu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 18, 2020 itakapotajwa tena.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )