Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 28, 2020

Lusinde 'Alipuka' Bungeni....Asema barabara kuelekea hospitali ya Mvumi imeoza

juu
Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde amesema hali ya barabara kuelekea hospitali ya Mvumi imeoza hivyo ni hatari kwa maisha ya watu.

Katika swali la nyongeza bungeni leo Jumanne Januari 28,2020, Lusinde amesema umuhimu wa hospitali ya Mvumi Mission unapotea na uzuri wa hospitali hiyo unakosekana kama hakutakuwa na barabara ya lami.

"Hata hiyo kilomita moja wanayosema imeanza kujengwa naona wamemdanganya Waziri, hakuna kitu, hali ni mbaya hasa kwa akina mama wanaohitaji huduma za hospitali hiyo na barabara nyingi nchi nzima zimeoza kabisa, nini mpango wa serikali katika eneo hilo," amehoji Lusinde.

Mvumi ndiyo hospitali kongwe kwa ajili ya wenye matatizo ya macho na kwa sasa ndiyo hospitali teule ya wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
 
Katika majibu ya serikali, Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Mwita Waitara amesema kutokana na umuhimu wa hospitali hiyo, wameanza maandalizi ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara hiyo.

Waitara amesema kwa kuanza wamepanga kujenga barabara hiyo kwa urefu wa kilomita moja kazi itakayokamilika Agosti 2020.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )