Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 28, 2020

Macho Yote ya Watanzania leo ni Kwa Mbwana Samatta!!

juu
Macho Yote ya Watanzania leo ni Kwa Mbwana Samatta  wakati atakaposhuka dimbani majira ya saa 4:45 usiku kuichezea timu yake mpya ya Aston Villa kwa mara ya kwanza, kwenye mechi ya Kombe la Ligi dhidi ya Leicester City katika Uwanja wa Villa Park.

Samatta alianza kujifua na wachezaji wenzake kwa mara ya kwanza Ijumaa iliyopita na Kocha wa Aston Villa, Dean Smith, alisema anaweza kuwa tayari kwa mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Ligi (Carabao Cup) dhidi ya Leicester City leo.

Hata hivyo, mashabiki wa Aston Villa wametakiwa kuwa watulivu kwa Samatta kwa kuwa haitakuwa rahisi kwake kuzoea ‘ligi hiyo ngumu zaidi duniani’.

Samatta, 27, ambaye alikamilisha uhamisho wake kutoka KRC Genk ya Ubelgiji kwenda Villa wiki iliyopita kwa takriban pauni milioni 8.5 hadi anaondoka alishacheka na nyavu mara 10 kwenye mashindano yote huku msimu uliopita akiifungia timu hiyo ya jumla ya mabao 42.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )