Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, January 2, 2020

Mbaroni kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mkewe

adv1
Na Amiri kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia ndugu Josphat Mtega (24) mkazi wa Ramadhani mjini Njombe kwa tuhuma za kumsababishia kifo  mkewe kilichotokana na ugomvi.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na kugombana na mkewe Angelina Sanga (24)  ambapo inadaiwa alimpiga na hivyo umsababishia majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake.

Kamanda anasema mara baada ya ugomvi huo, Angelina alisafirishwa hadi hospitali ya Ikonda iliyopo wilayani Makete  ambapo baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo uchunguzi wa kitabibu ulibaini kuwa dada huyo alionekana amevunjika mkono na sehemu mbali mbali za mwili wake zilionekana zimeshambuliwa vibaya.

Amesema mwanaume  huyo anaendelea kushikiliwa  na jeshi la polisi  kwa uchunguzi zaidi huku taratibu za kisheria zikiendelea.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )