Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 28, 2020

Serikali Yazungumzia Mlundikano wa Kesi Mahakamani

juu
Serikali  imetaja idadi ya kesi zinazotakiwa kusikilizwa kwa mwaka na majaji, mahakimu wa wilaya na wa mwanzo.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Januari 28, 2020 bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria,  Dk Augustino Mahiga na kubainisha kuwa ni mpango wa Serikali kuhakikisha kesi zote zinamalizika kwa wakati.

Amesema jaji mmoja anatakiwa kusikiliza kesi 220 kwa mwaka na hakimu wa Wilaya kesi 250 huku wale wa mwanzo wakitakiwa kusikiliza kesi 260.

Dk Mahiga amesema mahakama za rufani zimewekewa mkakati wa kumaliza kesi kwa muda usiozidi miaka miwili, mahakama za hakimu mkazi na wilaya zinatakiwa kumaliza kesi ndani ya mwaka mmoja na mahakama za mwanzo miezi sita.

Alieleza hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Mgogoni (CUF), Dk Ally Yusuf Suleiman aliyetaka kujua hali ikoje katika mahakama za Tanzania kuhusu mlundikano wa kesi.

Dk Mahiga amesema baada ya juhudi kubwa zilizofanywa na Rais John Magufuli, kwa sasa mlundikano wa kesi ni asilimia sifuri.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )