Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 14, 2020

Hospitali ya halmashauri ya ushetu suluhisho la wananchi kufuata huduma za afya umbali mrefu.

juu
SALVATORY NTANDU
Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa majengo ya saba ya  hospitali ya  halmashauri ya Ushetu wilayani kahama kwa asilimia 90 kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga imeagiza kuanza kutolewa kwa huduma za afya kuanzia mwezi machi mwaka huu ili kupunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta  za matibabu.

Hayo yalibainishwa febuari 10 mwaka huu na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa majengo ya hospitali hiyo na kumwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu, Michael Matomora kuhakikisha huduma za afya zinaanza kutolewa mwezi machi mwaka huu.

“Anzeni kutoa huduma za afya mara mmoja kwa kutumia majengo haya saba ya awali, tunataka wananchi wetu wapatiwe huduma hapa tunataka kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya halmashauri ya mji kahama ambayo ipo umbali wa zaidi ya kilomita 50 kutoka hapa nyamilangano”alisema Mlowa.

Alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kupitia ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2015/20 imeahidi kujenga zahanati kila kijiji na kituo cha afya kila kata ndio maana halmashauri hii ilipatiwa shilingi bilioni 1.5 kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Ushetu ambayo itatoa matibabu ya kibigwa katika ukanda huo.

Mlolwa aliongeza kuwa ni lazima wahakikishe wanatumia rasilimali watu ya watumishi wachache walionao kutoa huduma katika hospitali hiyo ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu sambamba kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa miundombinu ya barabara zote za eneo la hospitali hiyo.

Akitolea ufafanuzi kuhusiana na ujenzi wa hospitali hiyo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu Michael Matomora alisema kuwa watahakikisha mwenzi machi mwaka huu huduma za afya zinaanza kutolewa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za matibabu.

“Kwa mwaka huu wa fedha tumetenga bajeti ya shilingi milioni 500 ambazo zitatumika kukamisha baadhi ya miundombinu ya hospitali hii na tumejipanga kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) na huduma za akinamama na watoto ambazo sisi tuzipa  kipaumbele katika hatua za awali za kutoa huduma za matibabu”alisema Matomora.

Matomora aliongeza kuwa Halamshauri hiyo inayodawa za kutosha na vifaa tiba ambavyo vinatosheleza kuanza kutoa huduma za matibabu kwa kuanzia na watatumia watumishi wachache waliopo katika halmashauri hiyo.

Kuanza kutolewa kwa huduma za matibabu katika hospitali ya ushetu itapunguza msongamamo wa wagonjwa katika hospitali ya mji kahama ambayo inahudumia wagonjwa wa nje zaidi ya elfu 1000 kwa siku kutokana na kuhudumia halmashauri za Mbogwe,Msalala,Ushetu na Nzega.

Mwisho.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )