Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 17, 2020

Kabendera Kuendelea Kusota Rumande.....Ni Baada ya Hakimu Kupata Udhuru leo

juu
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa habari, Erick Kabendera imekwama kuendelea katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya hakimu anayeisikiliza, Janeth Mtega kupata udhuru

Kwa mujibu wa ratiba ya kesi hiyo leo ilitegemewa kuwa ni hatma ya mwisho ya Kabendera kusota rumande tangu alipopandishwa kizimbani Agosti 5,mwaka  2019 baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon  amedai mbele ya Hakimu Mkazi Vicky  Mwaikambo kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega anayesikiliza kesi hiyo hayupo hivyo ameomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, 2020 kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.Mil 173.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )