Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 18, 2020

Lukuvi amsimamisha kazi ofisa ardhi aliyetajwa na Rais Magufuli

juu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi amemsimamisha kazi ofisa ardhi wa Wilaya ya Kigamboni ambaye siku kadhaa zilizopita Rais Magufuli alitaka achukuliwe hatua kwa kuwa ni mtoro

Siku hiyo Magufuli alisema, “Nina tatizo na ofisa ardhi wa Kigamboni ni mtoro na hajafanya kazi karibu miezi mitatu, aliandikiwa barua na Wizara ya Ardhi ili ashughulikiwe ila bado wizara wanaleta mshahara wake. Najua wizara watafikishiwa ujumbe, kama ni mtoro atoroke kabisa, sifahamu mkurugenzi mmechukua hatua gani kwa ofisa ardhi huyo ambaye hafanyi kazi.”

Katika maelezo yake ya jana wakati akikabidhi ekari 715 za ardhi kwa manispaa ya Kigamboni kama alivyoagizwa na Rais Magufuli, Lukuvi alisema mtumishi huyo amesimamishwa kazi.

"Bahati nzuri  tulishapata barua kutoka kwa mkurugenzi wa Kigamboni na tumeshamsimamisha kazi wakati hatua za kinidhamu zikiendelea .Kama kutakuwa na uhitaji tutaleta mtu mwingine," alisema Lukuvi.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )