Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 10, 2020

Mfumuko Wabei Wa Taifa Wapungua Hadi Asimia 3.7%kutoka Asilimia 3.8%.

juu
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Mwezi Januari ,2020  umepungua hadi asilimia 3.7% kutoka asilimia 3.8% kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba ,2019.

Hayo yamesemwa leo Februari,10,2020 jijini Dodoma na Kaimu  mkurugenzi  wa Takwimu za  jamii na Sensa ya watu Bi.Ruth Minja wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema hii inamaanisha kuwa ,kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka  ulioishia Mwezi Januari,2020 imepungua  ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2019.

Bi.Minja amesema kupungua kwa  mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari ,2020 kumechangiwa na kupungua kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula  kwa kipindi kilichoishia  mwezi ,Januari,2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Januari,2019.

Aidha,Bi.Ruth ametaja baadhi ya bidhaa za vyakula zilizopungua bei  kwa mwezi Januari,2020 zikilinganishwa na bei za   mwezi Januari 2019 ni pamoja na Dagaa kwa asilimia 1.4,viazi kwa asilimia 3.4, magimbi kwa asilimia 7.1 na ndizi za kupika kwa asilimia 2.8.

Pia  amesema  mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilipungua bei kwa mwezi January 2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Januari 2019 ni pamoja na Gesi kwa asilimia 2,mafuta ya taa kwa asilimia 4.6,Petrol kwa asilimia 1.5 , Dozeli kwa asilimia 1.3 na majiko ya gesi kwa asilimia 4.6.

Amesema mfumko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi January 2020 umepungua hadi asilimia 5.7 kutoka asilimia 6.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2019.

Hata hivyo amebainisha  hali ya mfumko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2020 kwa Nchini kenya mfumko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2020 umepungia hadi asilimia 5.78 kutoka asilimia 5.82 kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2019.

Amesema kwa upande wa Nchi ya Uganda mfumko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2020 umepungua pia hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2019.

Mwisho.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )