Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi NACTE imevifutia usajili vyuo saba ambavyo vimethibitika kuendesha mafunzo bila kukidhi vigezo na utaratibu.
Akitoa taarifa hiyo mbele ya wanahabari, Mkurugenzi wa Opresheni wa NACTE, Dr Geofrey Oleke amesema lengo la kuvifutia vyuo hivyo usajili ni kutaka vikamilishe taratibu ili kutoa elimu yenye manufaa kwa Watanzania kwa kufuata misingi.
Orodha ya vyuo vilivyofutiwa usajili ni pamoja na ERA Training College - Bukoba (REG/TLF/095), Azania College of Management - Dar es Salaam (REG/BMG/021), Time School of Journalism - Dar es Salaam (REG/PWF/013), Clever College - Dar es Salaam (REG/BTP/205P) na Aces College of Economic Science - Mwanakwerekwe, Zanzibar (REG/BPT/081P).
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )